Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama Bi. Diana Z Sonno anawatangazia wananchi wote wa Butiama kuwa, maonesho ya wakulima Mkoa wa Mara yatafanyika Tarehe 12 Sept, 2020 hadi Tarehe 15 Sept, 2020 kwenye viunga vya maonesho vya Mama MARIA NYERERE vilivyopo wilayani Butiama. Teknolojia mpya juu ya Vipando, Mifugo, Uvuvi na Misitu itatolewa siku ya maonesho hayo.
Aidha, siku hiyo ya Tarehe 12 Sept, 2020 hadi Tarehe 15 Sept, 2020 itakuwa ni siku ya Wanamara (MARA DAY), ambapo shughuli za upandaji wa miti na Bikoni itafanyika katika Kijiji cha Kirumi kando kando mwa mto Mara pamoja na eneo la maonesho ya Nanenane.Wageni na Viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Mara watakuwepo.
Wote mnakaribishwa kushiriki katika maonesho hayo.
Butiama District Council
Anuani ya posta: P.O.BOX 1207 BUTIAMA
Simu: 2622163
Simu: 0756357458
Barua pepe: ded@butiamadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Butiama.Haki zote zimehifadhiwa